Uingereza:Kujadili mswada wa kujiua

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bunge la mabwana nchini Uingereza

Askofu mkuu wa zamani wa Cantebury Lord Carey amesema kuwa ataunga mkono sheria ambazo zitahalalisha watu wanaougua kupitia kiasi nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujiua.

Katika taarifa yake ndani ya gazeti la Daily Mail Lord Carey ameondoa pingamizi yake dhidi ya mswada huo kufuatia hali inayowakumba watu wanaougua.

Lakini Askofu mkuu wa Cantebury anayehudumu kwa sasa Justin Welby ameutaja mswada huo kama ulio na makosa na hatari kubwa.

Wabunge wataujadili mswada huo siku ya ijumaa.

Mswada huo uliowasilishwa na mbunge wa chama cha leba Lord Falconer utawapa fursa watu wazima nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujitoa uhai.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lord Carey

Fursa hiyo itashirikisha wale walio na chini ya miezi sita kuishi.

Madaktari wawili watalazimika kuthibitisha iwapo mgonjwa anaugua kupitia kiasi na kwamba wameafikia uamuzi wao wenyewe wa kujitoa uhai.

Takriban wabunge 110 wameorodheshwa kuzungumza wakati bunge litakapojadili mswada wa wanachama binafsi siku ya ijumaa.

Wakati Askofu Lord Carey alipokuwa Askofu mkuu wa Cantebury, alikuwa miongoni mwa watu waliopinga mswada wa Lord Joffes wa kuwasaidia wagonjwa wanaougua kupitia kisia kujitoa uhai ambao ulipingwa katika bunge la mabwana mnamo mwaka 2006.

Anasema kuwa inawezekana kuwa mcha mungu na vilevile kuwasaidia wale wanaotaka kujitoa uhai.

lakini katika taarifa yake hii leo katika gazeti la Daily Mail Lord Carey alisema ''ukweli ni kwamba nimebadilisha uamuzi wangu''.