UN:Waliokufa Gaza wengi ni raia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Miili ya Wapalestina waliouawa kwa mashambulizi yanayofanywa na Israel

Umoja wa Mataifa umesema robo tatu ya Wapalestina waliouawa kwa mashambulizi ya ndege yanayoendelea yanayofanywa na Israel huko Gaza ni raia wa kawaida.

Maafisa wa Palestina wanasema raia mia moja ishirini wameuwawa tangu mashambulio kuanza.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Magari ya deraya yakiwa vitani

Israel imesema inafanya mashambulio hayo, ili kujaribu kuwazuia wapiganaji wa Hamas, ambao wamekuwa wakirusha mamia ya makomborakwenye ardhi ya Israel.

Israel inalaumu wapiganaji wa Hamas kwa kutumia raia kama ngao kwa kuweka vifaa vya kivita kwenye makazi ya watu.

Professor Manuel Hassassian mwakilishi wa Palestina nchini Uingereza, ameiambia BBC, Israel kwa kuwalenga Hamas hukutakwepa kuwadhuru raia.

Alisema idadi kubwa ya raia wamekufa siyo sababu Hamas inajificha kati ya raia, yaani inawatumia raia kama kinga.

Gaza, kwa hivo wanapowalenga Hamas kamawanavosema, wanawalenga wa-Palestina wote. Siyo Gaza peke yake.Katika Ufukwe wa Magharibi piya, Israil imekuwa ikiwauwa kiholela, na huko hakuna makombora yaliyolegwa dhidi ya Israil" Alisema Hassassian.