UN yataka Israil na Palestina kuzungumza

Haki miliki ya picha AFP
Image caption UN yaitaka Israeli na Wapalestina kurejelea mazungumzo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka Israeli kukomesha mashambulizi yake dhidi ya Palestina katika ukanda wa Gaza.

Baraza hilo limeafikiana kwa sauti moja kuagiza wapiganaji wa Palestina na Israel kurejelea mazungumzo huku ikibainika kuwa zaidi ya asilimia 70% ya wapalestina 133 waliouawa katika mashambulizi haya ya ndege za kijeshi za Isareili ni raiya bila ya silaha..

Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia utoaji misaada kwa wakimbizi wakipalestina UNWRA linasema kuwa kati ya idadi hiyo 28 ilikuwa ni watoto wachanga.

Msemajizi wa UNWRA , Adnan Abu Hasna, ameomba pande zote husika kukomesha mauaji hayo ya Wapalestina.

''Kutokana na kile tulichokishuhudia kwa macho yetu hapa Gaza Watoto wanauawa bila ya kuhusika kwa njia yeyote na mapigano haya .

Hawa watoto wameuawa wakiwa bila hatia yeyote .Sio haki wao kuuawa katika njia hii''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mabomu yakilipuka Gaza

Zaidi ya wapalestina 133 wameuawa katika siku tano ya mashambulizi ya ndege za kijeshi za Israili huku ripoti zikisema kuwa muda mchache uliopita (jumamosi) Wapalestina wengine 15 wameuawa katika mashambulizi mapya.

Israel kwa upande wake inasema kuwa maeneo ya Tel Aviv yameshambuliwa kwa makombora 90 baada ya kundi la Kislamu la Hamas kutishia kushambulia mji huu baada ya ndege za kijeshi za Isareli kuendelea kulipua maeneo ya Gaza.

Uamuzi huu ni wa Kwanza kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na Mashambulizi ya Gaza.

Israel imesema inafanya mashambulio hayo, ili kujaribu kuwazuia wapiganaji wa Hamas, ambao wamekuwa wakirusha mamia ya makomborakwenye ardhi ya Israel.

Israel inalaumu wapiganaji wa Hamas kwa kutumia raia kama ngao kwa kuweka vifaa vya kivita kwenye makazi ya watu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Asilimia 70% ya waliouawa ni raiya kwa mjibu wa UN

Professor Manuel Hassassian mwakilishi wa Palestina nchini Uingereza, ameiambia BBC, Israel kwa kuwalenga Hamas huwatakwepa kuwadhuru raia.

Alisema idadi kubwa ya raia wamekufa siyo sababu Hamas inajificha kati ya raia, yaani inawatumia raia kama kinga.

Gaza, kwa hivyo wanapowalenga Hamas wanawalenga wa-Palestina wote. Siyo Gaza peke yake.Katika Ufukwe wa Magharibi pia, Israil imekuwa ikiwauwa kiholela, na huko hakuna makombora yaliyolengwa dhidi ya Israil" Alisema Hassassian.