Libya:Waasi wakabiliana mjini Tripoli

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji katika uwanja wa ndege wa Tripoli nchini Libya

Kuna ripoti kwamba mapigano yamezuka nchini Libya karibu na uwanja wa kimataifa wa ndege katika mji mkuu wa Tripoli.

Afisa mmoja amesema kuwa kundi la wanamgambo la Zintan linalodhibiti uwanja huo na barabara inayoelekea katika eneo hilo lilishambuliwa na waasi waliotaka kuwafurusha katika uwanja huo.

Waasi hao wa zamani kutoka kundi la Zintan wanaunga mkono watu walio na msimamo wa kadri wanaopinga wanamgambo hao kuchukua mamlaka katika taifa hilo ambalo lina yumbayumba tangu kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Muamar Gaddafi mnamo mwaka 2011.