Papa:Sheria ya kutooa kutafutiwa sababu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Papa Francis wa kanisa katoliki duniani

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa anaamini sheria inayowazuia makasisi katika kanisa hilo kuoa huenda ikaondolewa kulingana na wakati.

Papa Francis amesema kuwa sababu za kuiondoa sheria hiyo ya miaka elfu moja na mia moja ipo na kwamba atazitafuta.

Katika mahojiano na gazeti la kitaliano ,la Republica ,papa Francis pia ameifananisha na ugonjwa wa ukoma hatua ya makasisi kuwanyanyasa kimapenzi watoto wadogo.

Amesema kuwa takriban asilimia mbili ya viongozi hao wa dini ikiwemo maaskofu pamoja na makadinali huwanyanyasa watoto kimapenzi,na kwamba yuko tayari kukabiliana na tatizo hilo kwa hali na mali.