Mkakati wa Amani kuinusuru Gaza

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Zaidi ya watu170 wamefariki Gaza na wengi kujeruhiwa katika mashambulizi ya sasa ya Israel

Israel na Kundi la Hamas nchini Palestina zimesema , zitazingatia mapendekezo ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza yaliyotolewa na Misri.

Chini ya mpango huo , makubaliano ya kusitisha vurugu hizo zilizodumu takriban wiki moja yatatekelezwa mapema hivi leo Jumanne.

Baraza la usalama nchini Israel limesema kuwa litajadili mapendekezo hayo mapema hivi leo.

Misri imeratibu mpangilio wa usitwaji huo wa mapigano huko Gaza ikipendekeza utekelezwe kwenye saa chache zijazo .

Mchakato huo umeafikiwa baada ya kikao cha dharura kilichofanywa Cairo kilichowaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa umoja wa mataifa ya kiarabu, the Arab league.

Kikao hicho kitaendelea asubuhi hii ili kufuatilia kwa karibu uwisilishwaji wa mapendekezo hayo kwa pande husika.

Hii ndio hatua ya kwanza na ya pekee, lakini muhimu sana, iliyochukuliwa kufikia sasa kujaribu kusitisha umwagikaji damu huko Gaza ambako idadi ya wa-Palestinian wanaokufa kutokana na mashambulio ya Israel inaendelea kuongezeka ikifikia zaidi ya 170 ,wengine wengi kujeruhiwa na makaazi kubomolewa na mali nyingi kuharibiwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mbali na mashambulizi ya angani dhidi ya Gaza, Israel imetishia kupeleka vikosi vya ardhini.

Hamas nayo imekuwa ikiIfyatulia Makombora Israel.

'Hamna vifo vilivyoripotiwa upande wa Israel.'

Vikao vya mazungumzo kati ya maafisa wa Misri na pande hizo kinzani vimepangwa lakini kila upande utakuwa na ratiba tofauti na hawataonana ana kwa ana.

Kimsingi pande zote mbili, Israelis na Palestinians hawajakubali moja kwa moja mapendekezo yaliyotolewa, lakini angalau wamekubali wanatathmini ili kuipa amani nafasi.

Msimamo wa Israel ni kuwa wameisambaratisha Hamas na wameshaharibu maeneo wanayotengenezea makombora yao.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema kauli hiyo inaashiria wako tayari kuzungumza.

Misri ndio inachukuliwa kuwa mpatanishi bora ingawaje Hamas bado haiiamini kwa dhati serikali ya sasa ya Misri.