William Hague wa UK ang'atuka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza W. Hague ang'atuka.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague ametangaza atajiondoa kutoka kwa wadhfa huo.

Hatua hiyo inakuja wakati Waziri mkuu wa nchi hiyo David Cameron anafanya mabadiliko makubwa katika serikali yake akijiandaa na uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwaka ujao.

Inatarajiwa nafasi ya Bw. Hague itachukuliwa na waziri wa sasa wa ulinzi Philip Hammond.

Image caption Waziri mkuu wa UK David Cameroon amefanywa mabadiliko makubwa serikalini

Bila kufafanua Chama cha upinzani cha Labour kimeyataja mabadiliko hayo kama 'ufyekaji wa wale wenye misimamo ya kadri'

Hague amekuwa mbunge wa Richmond, North Yorkshire kwa zaidi ya miaka 26.

Hata hivyo Bw. Hague anatazamiwa ataendelea kuhudumu kama kiongozi katika baraza la mawaziri na atang'atuka kutoka bunge la nchi hiyo hapo mwakani wakati wa uchaguzi mkuu.