Malala akutana na Rais Goodluck Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Malala na mmoja wa wazazi wa wasichana waliotekwa nyara Nigeria

Mwanaharakati mwenye umri mdogo raia wa pakistan Malala Yousafzai amekutana na rais wa Nigeria Goodlack Jonathan mjini Abuja.

Lengo la mkutano huo ilikuwa kwa Malala kushinikiza Rais Goodluck kuchukua hatua zaidi ili kuwakoa wasichana wa shule waliotekwa na kundi la wanmgambo wa Boko Haram mwezi April.

Tayari mwanaharakati huyo ashakutana na familia za wasichana hao kuwapa moyo na matumaini.

Boko Haram wametoa kanda ya video ya kusuta kampeni za kutaka kuachiliwa wasichana hao. Kundi limetaka kuachiliwa kwa wapiganaji wake.

Malala alipigwa risasi kichwani na kundi la Taliban nchini Afghanistan alipokuwa akipigania elimu kwa wasichana.

Malala mwenyewea alikuwa mwathiriwa wa vita vya Taleban nchini Pakistna ambao na wao pia wanapinga elimu kwa watoto wasichana.

Yuko nchini Nigeria kwa ziara ya siku tatu. Katika siku ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, ameamua kwenda Nigeria kutoa wito wa kuwachiliwa kwa wasichana hao wengi ambao wana umri sawa na yeye, miaka 17.

Ni miezi mitatu tangu wasichana hao zaidi ya 200 kutekwa nyara na pia sio kawaida kwamba Rais Jonathan bado hata hajakutana na familia za wasichana hao.