Marekani yaiwekea Urusi vikwazo zaidi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Obama ajaribu kuiadhibu Urusi akisema Moscow yaihujumu Ukraine, Je Atafanikiwa?

Marekani imetangaza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi ikilenga secta zake za Ulinzi, fedha na makampuni ya kawi.

Baadhi ya waliolengwa na vikwazo hivyo vikali ni kampuni kubwa ya mafuta , Rosneft,makampuni ya ulinzi na hata maafisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Urusi.

Rais Obama amesema ni kwa sababu utawala wa Moscow badala ya kuchukua hatua za kusaidia kumaliza mgogoro wa mashariki mwa Ukraine inaelekea inaendelea kuuchochea.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Putin asema vikwazo vya Marekani kwa Urusi ni mwiba utakaoichoma pia Marekani

Amesema Urusi ilitarajiwa ikomeshe upenyezwaji wa silaha na wapiganaji kutoka Urusi wenye lengo la kuendeleza mapigano huko mashariki mwa Ukraine.

Rais wa Urussi , Vladimir Putin, ambae kwa sasa yuko Brazil kwa mkutano wa kiuchumi wa mataifa ya Brics -- amejibu kwa kusema vikwazo hivyo vitaaathiri pia maslahi ya Marekani na kuzorotesha zaidi uhusianoo baina ya mataifa hayo.

Kwa upande wao Viongozi wa nchi za umoja wa Ulaya nao wamesema wataongeza vikwazo dhidi ya Urussi kwani inaendelea kuuhujumu utaifa wa Ukraine.

Ulaya na Marekani ni baadhi ya nchi zinazotegemea zaidi kawi ya gesi kutoka Urusi.