Libya yahofia kuporomoka

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Libya wana wakati mgumu kukabiliana na makundi ya wapiganaji wa kiisilamu

Libya imelionya baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba iwapo haitapata usaidizi wa kuimarisha vikosi vyake vya usalama taifa hilo litakuwa miongoni mwa mataifa yaliofeli.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Libya Mohammed Abdelaziz ameliambia baraza hilo kwamba taifa lake linahitaji wataalam kuwafunza maafisa wa polisi na wanajeshi ili kulinda miundo mbinu muhimu kama vile visima vya mafuta,bandari na viwanja vya ndege.

Ameliagiza baraza hilo kuchukua hatua za haraka iwezekanavyo.

kumekuwa na ongezeko la visa vya ghasia kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo nchini Libya na tayari umoja wa mataifa umewaondoa maafisa wake wa kimataifa kutoka taifa hilo.