Wahamiaji wafariki Utaliana

Pwani ya Utaliana Haki miliki ya picha THINKSTOCK

Taarifa kutoka Utaliana zinaeleza kuwa wafanya kazi za uokozi wamekuta maiti 19 kwenye mashua iliyowabeba mamia ya wahamiaji kutoka Afrika Kaskazini.

Shirika la habari la Utaliana, ANSA, linasema inavoelekea wanyonge hao walikosa hewa safi walipogubikwa na moshi wa injini kongwe chini ya deki.

Wahamiaji wawili kwenye mashua hiyo walinusuriwa kwa helikopta kupelekwa hospitali.