Je sabuni inaweza kurejesha ubikira?

Baadhi ya wanawake na wasichana huko nchini Kenya wanatumia sabuni inayodaiwa kurejesha usichana yaani 'ubikra'.

sabuni hizo zinadaiwa kukaza misuli ya sehemu za uke na hivyo kuimarisha raha wakati wa kushiriki tendo la ngono na mwanaume.

Baadhi ya wasichana waliohijiwa na BBC mjini Nairobi wamekiri kutumia sababu hiyo na kusema kuwa imeweza kubana misuli ya uke na kurejesha hali ya ubikira.

Hata hivyo mtaalam wa magonjwa ya wanawake kutoka nchini Tanzania anasema kutumia sabuni pamoja na kemikali nyingine kwenye uke ni hatari.

Mtaalam huyo amewashauri wanawake kuacha kutumia kemikali kwani pia inaweza kuwaletea magonjwa mengine kama vile saratani.