Cheyech ashinda dhahabu Glascow

Image caption Flomena Cheyech na Caroline Kilel

Mkenya Flomena Cheyech Daniel ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za marathon kwenye mashindano ya jumuiya ya madola mjini Glasgow.

Amemshinda Mkenya mwenzake Caroline Kilel aliyekuwa wa pili na kushinda medali ya fedha.

Kwa upande wa wanamme Michael Shelley kutoka Australian ameshinda medali ya dhahabu.

Amemtangulia Mkenya Stephen Chemlany.

Michael Shelley ametumia muda wa saa 2 dakika 11 na sekunde 15 akimzidi wa pili kwa sekunde 43.

Mganda Philip Kiplimo amenyakua nafasi ya tatu.

Matokeo ya mbio za wanaume

1. Michael Shelley Aus 02:11:15 2 Stephen Chemlany Ken 02:11:58 +0:43 3 Abraham Kiplimo Uga 02:12:23 +1:08 4 Munyo Solomon Mutai Uga 02:12:26 +1:11 5 John Ekiru Kelai Ken 02:12:41 +1:26 6 Erick Ndiema Ken 02:13:44 +2:29 7 Liam Adams Aus 02:13:49 +2:34 8 Philip Kiplimo Uga 02:14:09 +2:54