Papa aomba vita vimalizwe

Pope Francis Haki miliki ya picha AP

Papa Francis ameomba amani kwa dhati katika hotuba ya kila juma katika medani ya St Peter's mjini Rome.

Aliacha kusoma hotuba aliyoandika kuomba vita vimalizwe na hisia ikisikika kwenye sauti:

"makaka na madada, hapana vita, hapana vita, nawafikiria hasa watoto ambao wananyimwa matumaini ya maisha ya maana, ya siku za mbele, watoto waliokufa, walioumia, watoto walioachwa na vilema, waliokuwa yatima, watoto ambao wanacheza na mabaki ya vita, watoto wasiojua kucheka.

Acheni kupigana.

Nakuombeni kwa moyo wangu wote.

Tafadhali, acheni sasa hivi!"