Emirates yabadilisha safari za ndege

Image caption Shirika la ndege la Emirates labadilisha safari za ndege

Shirika la ndege la Emirates limesimamisha safari za ndege zake zinazopaa juu ya anga ya Iraq ikihofia kuwa mapigano yanayochacha nchini humo yanaweza kuleta mkasa kama ule ulioikumba ndege ya Malaysia ya MH17.Emirates Inasisitiza kuwa hatua hiyo iliyoichukua ni ya tahadhari tu .

Hata hivyo wadau wa ya maswala ya usafiri wa ndege wanasema kuwa bila shaka hatua hiyo inafwatia mkasa uliosababisha vifo vya watu 290 ndege ya Malaysia MH17 ilipotunguliwa katika anga ya mashariki mwa Ukraine.

Vyombo vya dola nchini humo zinainyoshea kidole cha lawama wapiganaji wanaotaka kujitenga ambao wanaungwa mkono na Urusi .

Emirates imesema kuwa itabadilisha barabara za ndege zake mara moja ilikuepuka kupaa juu ya Iraq.

Mwenyekiti wa shirika hilo Tim Clark amesema kuwa MH17 ilibadilisha kilakitu kinachohusiana na usafiri wa ndege zisizo za kivita.

Haki miliki ya picha reuters
Image caption Mabaki ya ndege ya Malaysia MH17

Clark anasema kuwa anatarajia Mashirika mengine zaidi ya ndege kuchukua hatua dhidi ya anga za mataifa yaliyovitani .

''Tunatarajia tangazo katika mkutano baina ya viongozi wa mashirika ya ndege huko Canada juma lijalo.

kwa sasa Usalama wa anga yeyote huamuliwa na serikali tawala jambo ambalo sasa linatiliwa shaka na matukio huko Ukraine, Syria,Libya Iraq Sudan na sehemu za Yemen na Somalia.