Wauawa kwa kushambuliwa na kombora

Haki miliki ya picha AP

Wizara ya afya katika ukanda wa Gaza imeeleza kuwa watu wapatao kumi wameuawa kutokana na shambulizi la makombora yaliyolenga viwanja vya michezo.

Wanaume wengine watatu nao walipigwa na mabomu hayo wakati wakiwa katika eneo la mashambulizi.

Kombora jingine lilitua katika jengo moja la hospitali ya Shifa na kusababisha madhara makubwa huku likitajwa kuwa ni kubwa kuliko yote mjini Gaza.

Kundi la Hamasi halikusita kutoa shutma na kuinyooshea kidole Israel kwa shambulio hilo, hata hivyo msemaji wa jeshi la Israel amesema wao pia walikoswakoswa kwa makombora katika kitovu cha Gaza.

Shambulio hili limekuja wakati ambapo sherehe za sikukuu ya Eid el fitri zikiadhimishwa baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki MOON ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo,na kusema kuwa pande zote mbili zinapaswa kuwajibika kwa matokeo ya maafa hayo.