Binamu wa Karzai auawa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hasmat Karzai

Binamu wa rais Hamid Karzai wa Afghanistan, Hashmat Karzai ambaye ana ushawishi mkubwa nchini humo, ameuwawa katika shambulizi la kujitoa mhanga kusini mwa mji wa Kandahar.

Msemaji wa gavana wa mkoa huo amesema Hashmat alifariki baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua, huku akimkumbatia katika kisingizio kwamba anampa Bwana Karzai salamu za sherehe za Eid Ul Fitri.

Image caption Hashmat Karzai na simba wake enzi ya uhai wake alikuwa mfugaji simba

Hashmat alikuwa mmmojawepo wa watu maarufu waliompigia debe Ashraf Ghani katika kampeni zake za uchaguzi mkuu zilizomalizika hivi majuzi.

Ashraf alikuwa ni mmoja wa wagombea urais wawili katika uchaguzi uliokuwa na utata mwezi uliopita.

Wanahabari wanasema Hashmat alikuwa na ushawishi mkubwa huko Kandahar na pia alifahamika kama mfugaji wa simba.