Silaha za Korea kaskazini zazuwiwa

Haki miliki ya picha AP

Umoja wa Mataifa umeiwekea vikwazo Kampuni ya Meli ya Korea Kaskazini ambayo ilikuwa ikiendesha Meli iliyokamatwa huko Panama mwaka jana ikiwa na shehena ya silaha.

Serikali ya Cuba ilisema ilikuwa ikizisafirisha silaha za zamani za kipindi cha Soviet ili zikakarabatiwe katika Korea Kaskazini kisha zirejeshwe lakini Balozi wa Marekani Samantha Powe aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa Kampuni hiyo ilikuwa ikijaribu kuvikwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Vikwazo vipya vina maana kuwa Kampuni hiyo sasa haitaweza kufanya shughuli yoyote kimataifa.