Mwanamke apigwa risasi Somalia

Haki miliki ya picha Getty

Taarifa kutoka Somalia zinasema mwanamke mmoja katika eneo la kusini mwa nchi hiyo ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kukataa kuvaa nikabu.

Ndugu ya mwanamke huyo wamesema wapiganaji wa Al Shabaab walifika kwa mwanamke huyo na kumwamuru avae nikabu.

Na waliporudi kuangalia kama agizo lao limetekelezwa na kukuta hajaivaa ndipo walipomuua kwa kupiga risasi.

Al Shabaab wamekana kumuua mwanamke huyo na kusema kuwa bado hawajatawala moja kwa moja eneo la Lower Juba mwanamke huyo anapoishi.

Kundi la Al Shabaab ambalo linatawala eneo kubwa la kusini na katikati mwa Somalia limeweka sheria kali ikiwemo namna ya uvaaji wa nguo kwa wanaume na wanawake.