UNICEF: Raia wapo hatarini Gaza

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi raia walioathirika eneo la Gaza

Mkuu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF kwenye ukanda wa Gaza anasema kuwa raia wengi wamo kwenye hatari kubwa.

Pernille Ironside amesema kuwa hali iliyopo imeibua wasiwasi kuhusu usalama kwa raia waliomo majumbani au hata kwenye shule kwani wanalengwa na Israeli.

Umoja wa mataifa unasema umelemewa, kwani mapigano yamedumu kwa majuma matatu sasa.

Unasema kuwa Israeli italazimika kubeba majukumu ya kuwahudumia zaidi ya watu laki mbili waliohama makwao.