Afrika Kusini Kuchunguza ajali ya Twiga

Haki miliki ya picha AP
Image caption twiga

Taasisi inayolinda haki za wanyama Afrika ya Kusini wanachunguza kifo cha Twiga ambaye hapo awali taarifa zilikuwa zikidai alijeruhiwa alipokuwa akisafirishwa kwa njia ya barabara.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Twiga huyo, mmoja kati ya wawili waliokuwa kwenye Lori, alijigonga kichwa kwenye Daraja.

Twiga wote wawili walipelekwa kufanyiwa uchunguzi lakini chombo cha serikali kinachozuia ukatili juu ya wanyama kimesem mmoja alikufa mara tu baada ya kufikishwa katika eneo la matibabu.

Tukio hili limezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Shuhuda, Thinus Botha aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kuwa alikuwa akiendesha nyuma ya Lori hilo akashuhudia namna Twiga huyo alivyojigonga kwenye Daraja la Garsfontein barabara ya N1 ya Johannesburg's.

Kulikuwa na damu nyingi, Thinus Botha aliandika.

Meneja wa chombo cha serikali kinachozuia ukatili juu ya wanyama Afrika ya Kusini, alikuwa amejeruhiwa kichwa chake lakini uchunguzi unapaswa kufanyika kujua chanzo cha kifo.

Amesema pia wanyama hao walikuwa wakisafirishwa kuelekea bustani ya wanyama iliyoko Warmbarths, kama Kilomita 160 yaani maili 99 nje ya Johannesburg.