Israel,Hamas kusitisha mapigano saa 72

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashambulizi Israel na Hamas

Marekani na Umoja wa mataifa wamesema Israel na Hamas wamekubaliana kusitisha mapigano kwa saa 72 katika Gaza kuanzia alfajiri leo Ijumaa.

Taarifa ya wizara Ya afya ya Gaza,tangu kuanza kwa mapigano julai 8 wapalestina 1,422 wameshauawa wengi wao wakiwa raia.

Israel nayo imepoteza wanajeshi 56 na raia wawili.

Israel inasema operesheni yake ndani ya Gaza imeundwa ili kuwalinda watu wake na mashambulizi ya majeshi ya Palestina.

Katika tamko la pamoja, Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon wamesema wakati huu wa usitishaji mapigano kwa saa 72 vikosi vitabakia katika eneo hilo na wakazitaka pande zote mbili kutulia bila kuyavunja makubaliano hayo lengo likiwa kuwapa nafasi wananchi wasio na hatia kutafuta maeneo ya kukimbilia kuzikwepa ghasia.

Karibia robo ya wakazi wa Gaza wamejikuta nje ya maeneo yao kutokana na ghasia hizo.