Marekani :Tunataka barua pepe Microsoft

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kampuni ya Microsoft

Mahakama nchini Marekani imeamuru kampuni ya Microsoft kukabidhi barua pepe zote zilizotunzwa katika kituo cha kampuni hiyo cha Ireland kwa madai kuwa taarifa hizo zinalihusu taifa hilo.

Jaji wa Mahakama hiyo amesema kuwa japo kuwa nyaraka hizo za barua pepe hazikuwa ndani ya nchi hiyo si hoja ya msingi kwa kampuni ya Microsoft kutokabidhi kwa Marekani.

Amesema cha msingi ni kwamba nyaraka hizo kwa kuwa zinaihusu Marekani basi zikabidhiwe bila kujali zimetunzwa nje ya taifa hilo.

Makampuni kadhaa katika kesi hiyo yanaegemea kwa kampuni ya Microsoft kuhofia kupoteza wateja wake iwapo barua pepe hizo zitapelekwa Marekani kwani itabainisha usalama mdogo wa siri za wateja wao.

Hata hivyo jaji wa kesi hiyo amewapa muda wa kutosha kampuni ya Microsoft kukata rufaa mahakama kuu.