Bunge la Libya lakutana nje ya Tripoli

Athari za mapigano ya LIbya Haki miliki ya picha EPA

Bunge la Libya lilochaguliwa karibuni limekutana kwa mara ya kwanza huku ghasia zinazidi nchini baina ya makundi ya wanamgambo yanayopingana.

Wabunge walikutana Tobruk ili kukwepa mji mkuu, Tripoli na mji wa Benghazi ambako kikao hicho kilipangwa kufanywa.

Watu zaidi ya 200 wameuwawa katika miji hiyo miwili katika majuma mawili yaliyopita.

Mapigano yalizidi katika eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli, ambako matangi ya mafuta yalichomwa moto juma lilopita, na sasa yamepigwa tena kwa makombora.

Ghasia hizo zimefanya nchi kadha kuwaondoa wanabalozi na raia wao Libya.