Shambulio lakiuka utu, asema Ban Ki Moon

Shule ya Umoja wa Mataifa ya Rafah Gaza iliyoshambuliwa na Israil Haki miliki ya picha AFP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameelezea shambulio la makombora karibu na shule ya Umoja wa Mataifa huko Rafah, Gaza, ambalo liliuwa watu kama 7, kuwa kitendo "kilichokiuka utu na ni cha uhalifu".

Wapalestina wanasema watu kama 10 waliuwawa.

Bwana Ban alitoa wito mapigano yasimamishwe haraka, na kusema "wazimu huu lazima usite"

Walioshuhudia tukio hilo wanasema shambulio hilo katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, lilifanywa na ndege za Israil.

Maelfu ya raia walikuwa wanapata hifadhi katika jengo hilo.

Msemaji wa serikali ya Israel, (Mark Regev) alikanusha kuwa Israel ililenga shule yenyewe.

Nchini Israil kwenyewe mazishi yamefanywa ya mwanajeshi, Hadar Goldin, ambaye Israil ilisema awali kuwa alitekwa nyara na Hamas.

Sasa inajulikana kuwa alikufa katika mapigano.