Mazungumzo ya Gaza yasusiwa

Wapalestina wa Gaza wanakagua kombora la Israil lisiloripuka

Ujumbe wa Wapalestina uko Misri kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano, lakini Israil inasema haitopeleka ujumbe huko.

Naibu waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Marekani, William Burns, akitarajiwa, lakini sasa inaarifiwa hatokwenda Cairo.

Wala mjumbe maalumu wa Mashariki ya Kati, Tony Blair.

Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema haikuelekea kuwa mafanikio yoyote yatapatikana katika mzungumzo hayo.