Sasa Jeshi lazuia watu kuingia Monrovia

Image caption Wanajeshi wa Liberia wameweka vizuizi kuzuia watu kutoka eneo lenye ebola kuingia Monrovia.

Wanajeshi wa Liberia wameweka vizuizi katika barabara kuu za kuingia na kutoka jijini Monrovia ilikuwazuia watu kutoka eneo la Magharibi mwa taifa hilo chimbuko la ugonjwa wa Ebola kutoingia katika mji mkuu.

Hatua hiyo inafuatia hali ya tahadhari iliyotangazwa na rais ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao kufikia sasa umeua zaidi ya watu 930 katika kanda ya Afrika Magharibi.

Katika nchi jirani ya Sierra Leone maafisa wa Usalama huko wameweka vizuizi na kuzuia kuingia ama kutoka katika maeneo ya Mashariki mwa nchi yaliyoathirika pakubwa na Ebola.

Image caption Sasa Jeshi lazuia watu kuingia Monrovia

Huko Uswisi wataalamu wa afya ya umma wanaendelea kujadili mstakabal wa afya ya umma chini ya nembo ya shirika la afya duniani WHO.

Moja ya mapendekezo ni kutangazwa kwa ugonjwa wa Ebola kuwa janga la dunia huku wengi wakipendekeza kutangazwa kwa hali ya tahadhari kote duniani kufuatia mlupuko huo magharibi mwa Afrika.

Marekani na mataifa ya ulaya imesema kuwa inatafuta mbinu za pamoja katika kutokomeza ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Ebola kwa nchi umebainika kuwepo Guinea, Sierra Leone na Nigeria ambapo zaidi ya watu 930 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Saudi Arabia pia imesema raia wa nchi hiyo aliyebainika kuwa na virusi vya Ebola alivyovipata Sierra Leone amekufa katika hospitali ya Jeddah ambapo ndiye muasiriwa wa kwanza wa Gonjwa hilo nje ya bara la Afrika.

Image caption Watu 930 wamekufa kutokana na Ebola

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametangaza kuwa janga la kitaifa ugonjwa huo ambao analaumu ukosefu wa ufahamu kuhusu inavyoeneo ugonjwa huo na pia viwango vya juu vya umasikini miongoni mwa Waliberia.

Mwandishi wa BBC Jonathan Paye-Layleh aliyeko kilomita 37 kutoka mji mkuu wa Liberia Monrovia amesema kuwa wanajeshi hao wamewanyima idhini wakaazi wengi wenye asili ya maeneo yaliyoathirika pakubwa wruhusa ya kuingia mjini.

Wengi wao ni wasafiri na fanyibiashara.