Ebola yazua hofu Nigeria

Haki miliki ya picha elvis
Image caption Ebola yazua hofu nchini Nigeria.

Chama cha madaktari nchini Nigeria kimetangaza kukamilika kwa mgomo wa kitaifa ulioanza karibu mwezi mmoja uliopita kutokana na kuwepo mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Watu wawili wameaga dunia na wengine watano wameambukizwa maradhi hayo nchini Nigeria taifa lililo na watu zaidi barani Afrika.

Hadi sasa takriban vifo 930 vilivyotokana na ugonjwa wa ebola vimeripotiwa nchini Liberia, Sierra Leone na Guniea.

Liberia nayo imetangaza hali ya tahadhari.

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleas amesema kuwa hatua zaidi zinahitajika ili kulioka taifa hilo.

Kasisi mhispania aliyeambukizwa ugonjwa huo akifanya kazi kwenye hospitali moja nchini Liberia amesafirishwa kwenda nchini uhispania kwa matibabu.

Image caption Madaktari wamesitisha mgomo wao ilikukabiliana na mlipuko wa Ebola.

Mkuwatano wa pili wa dharura kuhusu ugonjwa wa ebola umeingia siku ya pili kwenye makao makuu ya shirika la afya duniani WHO mjini Geneva.

Huko Nigeria juhudi zimeanza kunoga ilikukabiliana na tishio la mlipuko wa ugonjwa huo wa Ebola.

Vituo vya Radio mjini Lagos vinatoa ushauri kuhusu njia za kuwa salama ili kusaidia kuzuia kusambaa wa ugonjwa wa ebola.

Zaidi ya watu 930 wameaga dunia nchini Sierra Leone, Liberia, Guinea na Nigeria katika kile kinachotajwa kuwa mlipuko mbaya zaidi wa ugonjwa wa Ebola kuwai kushudiwa.

Wanajeshi wametumwa kwenda maeneo tofauti nchini Liberia kuzuia watu kutembea kutoka sehemu zilizoathiriwa na ugonjwa huo .

Nchini Liberia hali ya hatari imetangazwa na watu wengi walio wagonjwa wanarudi nyumbai bila kutibiwa baada ya madaktarti kukosa kufika hospitalini.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Daktari akijihami kuwatibu washukiwa wa Ebola mjini Lagos.

Nao mkutano wa pili wa dharura kuhusu ugonjwa wa ebola umeingia siku ya pili kwenye makao makuu ya shirika la afya duniani WHO mjini Geneva.