Wanandoa wa Canada wachunguzwa China

Image caption Kevin na Julia Garratt pamoja na watoto wao wawili

Mamlaka za China zinawatuhumu wana ndoa raia wa Canada wanaofanya biashara ya mgahawa nchini kwamba wanahusika na wizi wa siri za nchi kuhusiana na masuala ya utafiti wa kijeshi.

Wanandoa hao Kevin na Julia Garratt wanamiliki mgahawa wao katika mji wa Dangdong karibu na mpaka wa Korea Kaskazini.

Kevin na Julia kwa sasa wanafanyiwa uchunguzi na idara za usalama Kaskazini Mashariki mwa Dandong.

Mgahawa Kevin na Julia umekuwa maarufu kwa watalii na raia wengine wa China hasa wale wanataka kujifunza kiingereza.

Haijafahamika mara moja ni kwa jinsi gani wanandoa hawa wamekuwa wakiiba siri za nchi, ingawa mtandao wa umekuwa ukiwasaidia wageni kuvuka mpaka kwenda Korea Kaskazini.

Nchini China makosa ya wizi ya taarifa za serikali ni adimu kutokea, japo kuwa makosa yaliyo mengi nchini humo hukumu yake huwa ni kifo.