Gumzo kwenye mitandao ya kijamii

Image caption Mkewe rais wa Cameroon, Chantal Biya

Viongozi wa Afrika wamewasili nchini Marekani kwa mkutano na Rais Obama kuhusu maendeleo na ustawi wa bara la Afrika.

Lakini kilichowavutia wengi ni mtindo wa nywele wa mkewe Rais wa Cameroon Paul Biya, Chantal Biya.

Chantal mwenye umri wa miaka 43 haogopi kusemwa na wala hakuna mtu anayeweza kumyanfa abadili mtindo huo wake ambao umemfanya kusifika sana, sio Papa, mkewe Rais Obama au hata marais wengine.

Huo ndio mtindo wake daima.

Image caption Katia picha ya zamani kidogo Chantal akiwa na mke wa Rais Barack Obama, Michelle Obama

Ni mpambe na hata akiwa miongoni mwa wanawake wengine mashuhuri ni rahisi sana kumtambua hata kwa kufumba macho maana huhakikisha ameng'aa kama nyota.

Wengi wanasema kwamba akiwa anakutana na marais au wageni waheshimwa anapaswa ngalau kushukisha ushungi wake lakini baadhi wanasema kila mtu ana uhuru wa kuvalia anavyopenda.

Nini maoni yako? Je mtindo wa nywele wa mtu unasema chochote kumhusu mtu huyo?