UN yaonya kukosekana misaada Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption magari ya deraya huko Ukraine

Umoja wa mataifa umeonya juu ya hali mbaya ya kukosekana misaada ya kibinadamu huko mashariki ya Ukraine, ambako mapigano kati ya vikosi vya serikali na vile vya waasi waliosambaratika yakiendelea.

katika mkutano wa dharula wa baraza la usalama la umoja wa mataifa,mkuu wa kitengo cha misaada ya kibinadamu,John Ging, amesema kwamba bila ya kupatikana kwa suluhu ya kisiasa huko Ukraine mapigano hayo yatasababisha watu kuwa hatarini zaidi na idadi ya watu waliokufa kutokana na mapigano hayo itaongezeka.

Naye balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa,Vitaly Churkin,ameyashutumu majeshi ya Ukraine kwa kuzidisha mashambulizi na kuongeza kwamba raia wapatao elfu nane wa Ukraine wameikimbia nchi yao na kutafuta usalama huko Urusi tangu mapigano hayo yalipoanza.