Obama awaaga marais wa Afrika Marekani

Haki miliki ya picha Getty

Siku tatu za mazungumzo yaliyolenga mustakabali wa bara la Afrika yamemalizika mjini Washington Marekani.

Mkutano huo ulikuwa wa kwanza wa aina yake kati ya Marekani na viongozi wa Afrika na ulilenga kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na bara la Afrika.

Lakini kwa sasa mkutano umekamilika , nini kimefikiwa ? Nani amefaidika na kwa njia gani?

Viongozi wanajiandaa kundoka mjini humo na kwa mara nyingine kuongeza msongamano wa magari mjini DC.

Marais 40 wa Afrika walikwenda Marekani kuona kile ambacho Rais Obama alikuwa amewaitia katika jitihada zake za kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Afrika.

Waliondoka nchini humo wakiwa na mikataba ya uwekezaji ambapo makampuni ya Marekani yameahidi kuwekeza katika nchi zao.

Mikataba hiyo ni ya thamani ya dola bilioni 14 pamoja na ahadi ya Marekani kuimarisha uchumi na mataifa ya Afrika pamoja na mchango mwingine wa pesa ili kuimrisha miundo mbinu na upatikanaji wa kawin barani humo.

Swala la usalama na ulinzi pia limeangaziwa

Marekani sasa imejitolea kuunga mkono kikosi cha dharura cha Muungano wa Afrika pia itatoa vifaa zaidi na walinda amani nchini Somalia na katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Lakini jee makubaliano haya yote yanatoa nafasi kwa ushirikiano mpya?

Viongozi wa Afrika wanafahamu kuwa Marekani inashindana na China na mataifa mengine yaliyostawi kwa sababu tu ta kutaka kuwa na ushahwishi mkubwa Afrika.

Lakini hakluna Rais anayeweza kukosa kukubali msaada kutoka kwa nchi tajiri zaid duniani kwa hilo.

Rais Obama amesema kuwa mazungumzo aliyofanya na marais wa Afrika yalikuwa ya kweli na yalitoa fursa ya kuweza kusikilizana na kuelewana.

Lakini kikubwa ni je mazikilizano hayo yatageuzwa na kuwa ya faida kwa washirika wote. The point now is whether that listening can be turned into action.