Israel yaanza kushambulia Gaza

Israel imeanza kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya Gaza katika hatua yake ya kujibu mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa kipalestina dhidi ya Israel.

Mashambulizi haya yametokea baada ya makubaliano ya siku tatu ya kusitisha vita kuvunjika.

Serikali ya Israel imesema kuwa iliamuru jeshi kujibu mashambulizi hayo kwa ukali.

Jeshi la Israel linasema linashambulia maeneo yanayotumiwa na wapiganaji hao katia ukanda wa Gaza.

Kuna taarifa za kutokea mlipuko mkubwa katika ukanda wa Gaza na wakazi wa Palestina wamekuwa wakiodnoka katika maeneo hayo.

Hamas ilikanusha madai ya kuongezwa muda wa makubaliano ya kusitisha vita ikisema kuwa Israel ilikataa kukubaliana kufanya mkutano kulingana na matakwa yao kwa masharti ya Misri ikiwemo kumaliza ,