AU itaunda kitengo cha magonjwa

Udhibiti wa Ebola, Nigeria

Mwenyekiti wa Hamashauri ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, ametoa wito kwa nchi za Afrika na duniani kote kushirikiana kuzuwia ugonjwa wa Ebola uliosambaa Afrika Magharibi, usitapakae kwengineko.

Shirika la Afya Duniani, WHO, linakisia kuwa watu kama 960 wamekufa kutokana na Ebola huko Guinea, Sierra Leone, Liberia na Nigeria.

Nkosazana Dlamini-Zuma alisema nchi za Afrika zinataraji kuunda kitengo cha pamoja kupambana na ugonjwa huo:

"Nchi za Afrika zimefikia uamauzi kuwa tunataka kuanzisha kitengo cha kudhibiti magonjwa.

Na tutafanya kazi pamoja na washirika wetu.

Marekani imekwishasema kuwa iko tayari kushirikiana nasi, lakini siyo pekee.

Lazima tushirikiane sana na WHO katika swala hili na washirika wengine walio tayari kuwa nasi"