Obama awataka viongozi Iraq waungane

Haki miliki ya picha AP
Image caption Obama awataka viongozi Iraq waungane ilikupambana na Islamic State

Rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuwa hakuna njia rahisi ya kuisaidia serikali dhaifu ya Iraq kukabiliana na wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State.

''Itachukua muda mrefu kwa majeshi yetu kuisidia Iraq kuwashinda wapiganaji wa Kisunni ambao wametangaza himaya yao inayojumuisha ardhi katika mataifa ya Iraq na Syria ''Alisema Obama.

Haki miliki ya picha REUTERS US NAVY
Image caption Majeshi ya Marekani yashambulia Wapiganaji Islamic State

Obama alisema kuwa itawabidi viongozi wa Iraq kuungana ilikupambana na Islamic State.

Rais Obama aliruhusu majeshi yake kuishambulia ngome ya Islamic State Ijumaa kwa mara ya kwanza ambapo majeshi ya Marekani imehusika katika vita moja kwa moja nchini Iraq tangu mwaka wa 2011.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wakimbizi kutoka jamii ya Yazidi wakitorokea maisha yao

Mashambulizi hayo dhidi ya wapiganaji wa IS iliharibu uwezo wao wa kuwashambulia jamii ya Yazidi ambayo ilikuwa imetorokea milima ya Sinjar baada ya Islamic State kuteka mji wa Qaraqosh.

Mapema leo ndege za kijeshi za Uingereza zimefunga safari kusaidia utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Iraq.