Riek Machar azuru Khartoum

Riek Machar Haki miliki ya picha Reuters

Kiongozi wa wapiganaji wa Sudan Kusini, Riek Machar, amefanya mazungumzo mjini Khartoum na Rais Omar al-Bashir wa Sudan.

Hiyo ilikuwa ziara yake ya mwanzo huko tangu mapigano kuanza baina ya wapiganaji wake na majeshi ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini mwezi Disemba.

Khartoum imejitenga na mzozo huo.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyowekwa na Jumuia ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, IGAD, ili kumaliza vita na kuunda serikali ya pamoja, yamemalizika Jumapili.

Ulimwengu umelaani mapigano ya Sudan Kusini ambayo yameingiza nchi kwenye njaa.

Mazungumzo yaliyoandaliwa na IGAD na yaliyofanywa mjini Addis Ababa, Ethiopia, hayakumaliza mzozo wa Sudan Kusini.