Raia wa Uturuki kumchagua rais mpya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uchaguzi nchini Uturuki

Raia wa Uturuki wanapiga kura hii leo kumchagua rais wao moja kwa moja kwa mara ya kwanza.

Hadi kufikia sasa bunge ndilo ambalo limekuwa na uwezo wa kumchagua kiongozi huyo wa taifa.

Wagombea walio kifua mbele katika uchaguzi huo ni waziri mkuu wa sasa Reccep Teyip Erdowan ambaye waandishi wanasema amekuwa akitawala siasa za taifa hilo.

Makundi ya kijamii yamekuwa yakizozana na chama cha Haki na maendeleo cha Erdowan kilicho na mizizi ya kiislamu.

Bwana Erdowan anataka wadhfa wa urais kupewa mamlaka mengi.

Wapinzani wake ni Mwanadiplomasia wa siku nyingi Ekmedddin Ihsanoglu pamoja na wakili Selattin Demirtas kutoka kabila la kikurdi walio wachache.