Maambukizi mapya ya Ebola Nigeria

Image caption Idadi ya waliofariki kutokana na Ebola yazidi kuongezeka Afrika Magharibi

Waziri wa afya nchini Nigeria amethibitisha visa kumi vya ugonjwa wa Ebola.

Onyebuchi Chukwu amesema kuwa visa hivyo vimepatikana katika mji mkuu wa lagos.

Wagonjwa wote walishikana na raia wa Liberia ambaye alizimia alipowasili katika uwanja wa ndege nchini humo na kufariki baadaye.

Bwana Chukwu amesema kuwa kisa cha hivi karibuni ni kile cha muuguzi aliyemtibu mgonjwa huyo.

Mjini Geneva Shirika la afya duniani linafanya mkutano wa wataalam wa matibabu ili kujaribu utumizi wa matibabu mapya.Watajaribu kutumia dawa ambazo hazijatumiwa na binaadamu.