Polisi wa Misri watuhumiwa kwa mauaji

Haki miliki ya picha Getty

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limesema kwamba vikosi vya askari wa Misri viliua idadi kubwa sana ya wananchi kuwahi kushuhudiwa ndani ya siku moja mwezi Agosti mwaka jana.

Idadi hii inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani.

Kwa muujibu wa taarifa zilizotolewa na kikundi hicho cha utetezi wa haki za binaadamu zinaeleza kwamba mauaji hayo ya waandamanaji waliokuwa wanampinga Raisi Mohammed Morsi,raia wapatao mia nane waliuawa katika uwanja wa Rab'a mjini Cairo mnamo tarehe 14 mwezi August mwaka 2013.

Kadhalika shirika hilo la kutetea haki za binadamu linasema kwamba mauaji hayo ya raia ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu na kuwataka viongozi wenye dhamana wa Misri kutenda haki juu ya maisha ya raia hao.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa shirika hilo, Kenneth Roth ambaye alizuiliwa kuingia ndani ya nchi ya Misri mapema wiki hii na kueleza alichokishuhudia na kuyafananisha na mauaji hayo na yale yaliyowahi kutokea katika uwanja wa Tiananmen nchini China.