Urusi yapeleka msaada nchini Ukraine

Haki miliki ya picha
Image caption Mamia ya watu nchini Ukraine bado wanakumbwa na hali ngumu ya kibinadamu

Urusi inasema kuwa karibu malori 300 yaliyosheheni misaada ya kibinadamu yameondoka mjini Moscow kuelekea mashariki mwa Ukrain kufuatia makubaliano na Ukrain ya kuwepo msaada wa dharura chini ya uongozi wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.

Vyombo vya habari nchini Urusi vinasema kuwa msaada huo utapokelewa kwenye mpaka na Ukrain na shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na kupelekwa kwa raia waliojipata kwenye mapigano mashariki mwa Ukraine.

Lakini shirika la Red Cross linasema kuwamaelezo kuhusu mpango hauo bado hayajatolewa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amesema kwamba lazima ihahakikishwe kwamba hatua hiyo ya Urusi sio njamaya Urusi kutaka kuingilia hali katika eneo hilo.