Kesi ya Kanali Egangela ni jaribio DRC

Image caption Umoja wa Mataifa wasema keshi dhidi ya mkuu wa jeshi nchini DRC ni jaribio

Wajumbe wa umoja wa kimataifa wamesema kuwa Kesi za kivita zilizoanza Jumatatu katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC zinazotarajiwa kuendelea kwa muda wa wiki tatu dhidi ya waliokuwa maafisa wa kijeshi itakuwa jaribio kwa haki za wanajeshi na wanaiangazia kwa umakinifu

Luteni kanali Bedi Mobuli Egangela aliyekuwa kamanda wa zamani amehukumiwa kwa mauaji,ubakaji pamoja na mateso anazodaiwa kutenda kati ya mwaka wa 2005-2006 mashariki mwa nchi hiyo.

Mwakilishi wa umoja wa kitaifa Campell alieleza BBC kuwa kesi hii inaashiria uzito wake ingawa mtuhumiwa amekataa madai haya.

Mgogoro mashariki mwa nchi hiyo umeendelea hata baada ya vita za wenyewe kwa wenyewe kuisha kwani vikundi vinangagania kudhibiti maeneo yenye madini.

Image caption Kesi hiyo huenda ikatoa mtizamo tofauti ya mizani ya haki DRC

Kanali Egangela alikuwa kiongozi wa majeshi baada ya kujiunga na wengine kama mpango wa kuleta amani na hatimaye akawa kamanda wa kikosi cha 106.

Kabla ya kujiunga na jeshi anasemekana kuajiri watoto kama wanajeshi na kuagiza mashambulizi katika vijiji vilivyo kusini mwa jimbo la Kivu na matusi kwa wanainchi alipokuwa kamanda wa wanajeshi.

Baadaye alitoka kwenye jeshi na kujiunga na waasi wa Mai waliopinga wazalendo.

Mwandishi wa BBC Maud Jullien akiwa jijini Kinshasa anasema kuwa kesi hiyo inawahusia wanajeshi 39 wa cheo cha chini waliohukumiwa kwa ubakaji na kuongeza matumaini kuwa haki itatendwa lakini wawili tu ndio walipatikana na hatia