Mubarak akana kuamrisha mauaji Misri.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mubarak akana kuamrisha mauaji Msiri.

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak amekana kuwa hakuamrisha maafisa wa Usalama wawashambulie waandamanaji mwaka wa 2011.

Mubarak mwenye umri wa miaka 86 alijitetea kuhusu vitendo vyake katika kesi inayomkabili akisema kuwa hakuagiza mauaji ya mamia ya waandamanaji .

Akizungumza kwa mara ya kwanza mahakamani ,Mubarak alikiri kufanya makosa kama rais ,lakini akasema kuwa alijitahidi kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Mubarak amesema kuwa alikubali kuwacha mamlaka mnamo mwaka 2011 ili kuzuia umwagikaji wa damu.

Bwana Mubarak alikuwa akizungumza katika kesi yake ambapo anashtakiwa kwa kupanga njama ya kuwaua mamia ya waandamanaji.

Mubaraka aliondoka malakani baada ya siku 18 ya maandamano huku watu zaidi ya 350 wakiwawameuawa katika makabiliano na vyombo vya usalama.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mubarak akana kuarisha mauaji Msiri.

Alikuwa amehudumu kwa zaidi ya miaka 30 kama rais wa Misri.

Rais huyo wa zamani alipatikana na hatia miaka mitatu iliyopita lakini uamuzi huo ukabatilishwa mwaka uliopita.

Kesi itaamuliwa tarehe 27 mwezi septemba.

Mubaraka alihutubia mahakama kwa takriban dakika 25 akiwa katika kiti chake cha magurudumu .

Aliiambia mahakama kuwa alikuwa ameitumikia serikali ya misri maisha yake yote lakini anastaajabu kwanini wakati wake wa mwishomwisho ndipo anapohangaishwa.

Kulingana naye anauhakika kuwa nafsi yake ni shwari.