Afutiwa kosa la kutorosha pesa Syria

Image caption Nawal aliambia mahakama kua alishauriwa kubeba pesa hizo na rafiki yake bila kumweleza zilikokuwa zinakwenda

Mahakama nchini Syria imefutilia mbali kesi ya mwanamke aliyeshitakiwa kwa madai ya kutorosha pesa kwenda Syria kwa kuzificha katika nguo ya ndani.

Ila rafiki yake amepatikana na hatia ya kosa la kufadhili ugaidi.

Mwanamke huyo kwa jina Nawal Msaad alituhumiwa kwa kutorosha pauni 15,800 ndani ya nguo zake za ndani kuingia nchini Syria, amefutiwa makosa baada ya kukosekana ushahidi.

Nawal Msaad, mwenye umri wa miaka 27, kutoka London, alisimamishwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow alipokuwa anajaribu kupanda ndege kwuelekea mjini Istalbul nchini Uturuki.

Pesa hizo inadiwa alidhamiria kumpwa mwanamke raia wa Uingereza,nchini Syria.

Mwenzake Amal El-Wahabi, mwenye umri sawa na wake, alituhumiwa kwa kosa la kujaribu kuingiza pesa Syria kimagendo kwa lengo la kufadhili ugaidi.

Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mumewe El-Wahabi alijiunga na wapiganaji wa kiisilamu nchini Syria.

Bi Msaad, alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Metropolitan mjini London akisema kuwa alikuwa amehadaiwa na mwenzake El-Wahabi.

Alisema alificha pesa hizo ili zisiibwe lakini akasema aliziingiza katika nguo yake ya ndani tu kwa sababau hiyo.

Mahakama ilimpata na hatia El-Wahabi kwa kumshawishi rafiki yake kubeba pesa hizo ili kumkabidhi mumewe aliye vitani nchini Syria.

Alipoachiliwa na mahakama aliangua kilio na kuondoka kwa haraka mahakamani huku mwenzake akipatikana na hatia na huenda akafungwa jela kwa miaka 14.