Obama atetea mashambulizi dhidi ya IS Iraq

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wakurdi wateka bwawa la Mosul kwa ushirikiano na Marekani

Rais Obama amesema kuwa Mashambulizi ya hewani yanayofanywa na Marekani dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu nchini Iraq yanapania kuchukua tena udhibiti wa bwawa kubwa zaidi nchini humo ili kulinda maslahi ya Wamerekani.

Obama alisema kuwa kutekwa kwa bwawa la maji linalotegemewa kwa maji ya mji wote mkuu wa Mosul ni hatari kwa wanajeshi wa Marekani walioko karibu huko.

Kauli hiyo ya Rais Obama ya kutuma wanajeshi wa Marekani kwa mara ya kwanza kuwasaidia wanajeshi wa Kurdi ambao sasa wanadhibiti bwawa hilo kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State ni hatua ya kwanza ya kuisaidia .

Iwapo tukio hili litathibitishwa itakuwa mabadiliko makubwa zaidi kufanywa na Marekani tangu wapiganaji wa Islamic state kuanza kufanya mashambulizi mwezi Juni.

Bwawa hilo ndilo linalotoa maji na umeme kwa mji wa Baghadad na miji mingine midogo nchini Iraq.

Hapo Jumapili Bwana Obama alieleza bunge la Congress kuwa operesheni yao nchini Iraq itakuwa fupi na ya kulengwa.

Obama alisema kutekwa kwa bwawa hilo kungezuia serikali ya Iraq kutowahudumia wananchi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bwawa la Mosul ndilo linalotoa maji na umeme kwenda Baghdad

Jeshi la Marekani limesema lilitekeleza mashambulizi 14 Jumapili na kuharibu magari 19 ya IS pamoja na kituo cha uchunguzi karibu na bwawa hilo.

Kundi linalopigania haki za binadamu limesema kuwa wanamgambo wa IS katika jimbo la Raqqa nchini Syria walilenga wanajeshi wa Syria.

IS ilitwaa maeneo makubwa ya ardhi nchini Iraq na Syria katika miezi ya hivi karibuni na kusababisha maelfu ya wakristo na watu wa dhehebu ya Yazidi kutoroka.

Waziri wa kigeni anayeondoka mamlakani Hoshyar Zebari aliambia BBC kuwa majeshi ya Peshmerga yalikuwa yamekabiliana na upinzani mkali katika vita vya kutwaa bwawa hilo.

Lengo lao kuu kwa sasa ni kuwafurusha wapiganaji wa ISIS kutoka Nineveh ili kuhakikisha jamii ya wachache kama Yazidi wamerudi makwao.

Haki miliki ya picha
Image caption Wapiganaji wa Peshmerga wanaodhibiti bwawa hilo la Mosul

Nchi za Magharibi zinaendele kutoa msaada wao kwa wakimbizi wengi ambao wako kwenye maeneo ya wakurdi.

Majeshi wa IS wanatuhumiwa kwa mauaji ya mamia ya watu wa Yazidi na wakristu wachache kaskazini mwa Iraq na Mashariki mwa Syria.

Inakisiwa kuwa watu themanini kutoka dini ya Yazidi wanaaminika kuuwawa na wanawake na watoto kutekwa nyara katika kijiji cha Iraq hapo Jumatano

Mapigano haya yametawanya watu milioni moja na laki mbilin chini Iraq pekee.

Waziri mkuu wa mpya wa Iraq Haider-Al-Abadi mwenyewe mShia anakumbana na changamoto la kuwaunganisha watu wenye imani ya Kisuni ambao hawana imani tena na serikali ya IRaq.