Mahakama yaaafiki marufuku ya Suarez.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mahakama ya rufaa ya michezo imeafiki marufuku ya miezi 4dhidiya Luis Suarez.

Mahakama ya rufaa ya michezo imeafiki marufuku ya miezi miine aliyopewa mshambulizi wa Barcelona na Uruguay Luis Suarez.

Hata hivyo Suarez amepata afueni kwani sasa ataruhusiwa kushiriki mazoezi na timu yake ya Barcelona

Wakili wa Suarez alifaulu kuishaiwishi mahakama kuwa Kauli ya FIFA ilikuwa kali kupindukia.

Shirikisho la soka duniani FIFA ilimpata na hatia Suarez kwa kumn'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipokuwa ikikabiliana na Italia katika kombe la dunia huko Brazil.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Suarez hata hivyo ameruhusiwa kuchapa zoezi na Barcelona

Kufuatia uamuzi huo Suarez, 27, atarejea katika mechi dhidi ya mahasimu wao Real Madrid ''El Clasico'' tarehe 26 Oktoba.

Mshambulizi huyo wa Uruguay ataendelea kutumikia marufuku ya mechi za kimataifa .