Msaada wa Urusi waelekea mpakani

Image caption Msafara wa msaada kutoka Urusi waelekea mpakani.

Msururu wa magari takriban lori 300 yalisimama usiku kucha katika mji wa kusini wa Voronezh na unatarajiwa kufika mpakani Ukraine baadaye jumatano.

Haijatambulikia bado vile msaaada huo utapeanwa huku kukiwa na hofu kwamba Urusi inaweza tumia msururu huo kama kisingizio cha kuchukua hatua za kijeshi nchini Ukraine.

Waziri wa mambo ya ndani Ukraine alisema msaada huo haungeruhusiwa kuingia nchini humo.

Arsen alisema katika ukurasa wake wa facebook nchini Urusi kwamba uchochezi na uchokozi wa kijinga hauruhusiwi katika eneo lao.

Image caption Msafara wa msaada kutoka Urusi waelekea mpakani.

Takriban watu 1,500 wameaga tangu kati ya mwezi wa Aprili wakati ambapo Ukraine ilituma majeshi yake dhidi ya waasi wasioiunga mkono Urusi katika maeneo ya Donetsk and Luhansk.

Mapigano hayo yamelazimu kuhamishwa kwa zaidi ya watu 300,000 kutoka makazi yao wengi wao wakiwa wametorokea Urusi.

Wakati huo huo, rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa Crimea kwa mkutano siku ya jumatano na wanachama wa baraza la usalama.

Urusi iliimega Crimea kutoka kwa Ukraine mwezi machine hatua iliyo ibua raundi ya kwanza ya faini dhidi ya Moscow.

Maafisa wa Urusi wanasema kwamba msafara huo umebeba karibu toni 2000 ya msaada kutoka Moscow kuelekea Luhansk jumanne asubuhi.

Image caption Msafara wa msaada kutoka Urusi waelekea mpakani.

Televisheni moja ya Urusi ilionyesha mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na nafaka, vyakula vya watoto na madawa ambayo itaendea raia ambao wamezuiliwa katika eneo la mapigano lililoshikwa na waasi wasioiunga mkono Urusi.

Msururu huo ulikaa usiku kucha mjini Voronezh takriban kilomita 300 kutoka mahali ambapo palikuwa pamependekezwa kuvukiwa kwa mpaka ,wa Shebekino-pletnyovka kwenda kharkiv ndani ya Ukraine na kwa sasa unaendelea na safari yake.

Siku moja kabla ya bwana Avakov alisema msururu huo haungeruhusiwa kuingia Ukraine.

Maafisa kutoka Ukraine waliweka masharti mapya ya kui kuingia kwa msafara huo nchini humo.

Msemaji wa baraza la usalama Andriy Lysenko alisema kwamba msaada unafaa kupitia kituo cha mpaka ambacho kinadhibitiwa na serikali na uwe unakuja na maafisa wa msalaba mwekundu.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Makabiliano baina ya majeshi ya Ukraine na wapiganaji yanaendelea .

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov hapo jumanne alisema kwamba Moscow ilikuwa imeitikia masharti haya.

Alinukuliwa na shirika la habari la Itar-Tras akisema kwamba wamepokea ilani kutoka kwa upande wa Ukraine ikiwa na hakikisho kuhusu kujitayarisha kwao kupokea msaada huu.

Bwana Lavrov aliongeza kwamba madai ya ukraine msaada huo uhamishiwe kwa magari mengine mpakani yaliachwa kwa misingi ya kuwa msafara huo utaendelea na safari yao kwa nambari za usajili za urusi.

Lakini mwana habari wa BBC Daniel Sandford akiwa Moscow anasema kwamba majadiliano yanaendelea ili kubaini kama msafara huo utaruhusiwa kuingia Ukraine.

Maafisa wa magharibi wameeleza wasiwasi kwamba urusi inatumia msaada wa kiibinadamu kama kisingizio chaa kuweka vikosi vyake mashariki mwa Ukraine.

Katibu mkuu wa nato Anders Fogh Rasmussen alionya hapo jumatatu kwamba warusi walikuwa waenendeleza simulizi na singizio la operesheshi ya kijeshi chini ya kivuli cha msaada.