Arejesha tuzo kwa mauaji ya Gaza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tuzo alipewa Zanoli

Raia mmoja wa Uholanzi aliyepewa tuzo na Israel kwa kumficha mtoto mmoja wa kiyahudi wakati wa vita vya dunia vya pili amerudisha medali aliyopewa baada ya ndege moja ya kijeshi ya Israel kuiharibu nyumba ya wakwe wa mpwa wake mkubwa.

Watu sita wa familia hiyo waliuawa.

Henk zanoli ambaye ana umri wa miaka 91 na mamaake walipewa tuzi hiyo inayopewa watu wasio wayahudi ambao hueka maisha yao hatarini kuwalinda wayahudi kutoka kwa watu Wa Nazi.

Bwana Zanoli ameliambia gazeti la Haaretz kwamba kwa kuhifadhi tuzo hiyo itakuwa ni kuwatusi watu wa familia hiyo waliouawa katika eneo la Gaza.