KQ yavunja safari za Afrika Magharibi

Mkurugenzi mkuu wa Kenya Airways, Titus Naikuni (kulia)

Shirika la ndege la Kenya limetangaza kuwa litasimamisha safari za ndege za kwenda Sierra Leone na Liberia kwa sababu ya ugonjwa wa ebola ulioko Afrika Magharibi.

Imesema hatua hiyo itaanza kutekelezwa kutoka usiku wa Jumaane.

Ndege zake zitaendelea kwenda Nigeria.

Akizungumza kwenye mkutano huohuo wa waandishi wa habari mjini Nairobi, mkurugenzi wa afya ya jamii, Nicholas Muraguri, alisema hakuna raia kutoka nchi zenye ebola atayeruhusiwa kuingia Kenya.

Shirika la afya duniani, WHO, limesema Kenya iko katika hatari ya ugonjwa wa ebola kuingia nchini humo, kwa sababu ni nchi ambapo safari nyingi za ndege kutoka Afrika Magharibi zinatua.

WHO piya ilisema makisio ya ugonjwa huo ulivotapakaa siyo kadiri ya hali halisi.