Wanavijiji wanusuriwa na jeshi la Chad

Image caption Wanajeshi wa Chad

Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa vikosi vya serikali ya Chad vimewanusuru wanavijiji 85 ambao walitekwa nyara mapema wiki hii katika mashambulizi makali yaliotekelezwa na kundi la Boko Haram.

Ripoti moja inasema kuwa vikosi vya Chad viliyasimamisha mabasi kadhaa yaliokuwa yakiwasafirisha wapiganaji na wanavijiji hao katika ukaguzi wa mara kwa mara .

Walionusurika katika shambulizi la jumapili iliopita wameiambia BBC kwamba wapiganaji hao waliwaua takriban watu 28 na kuwajeruhi wengine wengi kabla ya kuwateka na kuwavusha ziwa Chad wakitumia maboti.

Kundi la Boko Haram ambalo linataka kubuni taifa la kiislamu katika eneo la waislamu wengi la Kazkazini mwa Nigeria limeshtumiwa kwa kuwatekanyara mamia ya watu ili kuwatumia kama wanaosajiliwa kwa nguvu kujiunga na jeshi,mabibi zao pamoja na kuwa watumwa.

Zaidi ya wasichana mia mbili waliotekwanyara na kundi hilo hawajulikana waliko.