Gaza:Mazungumzo yaendelea

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mazungumzo ya Amani kati ya Israel na Palestina

Wajumbe wanaowakilisha Israel na Palestina wanatarajiwa kukutana katika mji mkuu wa Cairo nchini Misri siku ya jumapili ili kuendelea na mazungumzo yao yasio ya moja kwa moja kutafuta mwafaka wa kusitisha vita katika eneo la Gaza.

Pande zote mbili zinatekeleza makubaliano ya siku tano ya kusitisha vita yanayokamilika siku ya jumatatu usiku.

Siku ya Alhamisi wakati mazungumzo yalipokwisha wawakilishi wa Palestina walisema kuwa wanachukua tahadhari kuhusu maendeleo ya mazunngumzo hayo.

Kundi la wapiganaji wa Hamas linataka Israel na Misri kuondoa vikwazo vya mipakani dhidi ya Gaza huku Israel ikilitaka kundi la Hamas kusalimu silaha zao.